ROMBO, KILIMANJARO
ZAIDI ya Tembo tisa wamevamia kijiji cha Mahida Mangoni
wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, na kuua mtu mmoja na kujeruhi pamoja na kuharibu mazao ya migomba.
Mkuu wa wilaya hiyo Elinasi Pallangyo alisema tembo hao
waliigia kjijini hapo na kuanza uharibifu huo haliiliyopekea wananchi kuanza
kuwafukuza na hatimae tembo hao kuua mtu mmoja pamoa ja kujeruhi.
Alisema baada ya tembo hao kuua wananchi mmoja na kujeruhi,
wananchi hao waliwashambulia tembo hao na kuua tembo mmoja.
Mkuu huyo amewataka wananchi wilayani humo kutosumbua
wanyama hao pindi wanapoingia ndani ya wilaya hiyo na badala yake kutoa taarifa
kwa vituo vya askari vya wanyama pori
vilivyopo wilayani humo.
Kamanda wa polisi
mkoani hapa Robert Boaz amethibitisha kutokea kwa kutukio hilo na kwamba
lilitokea agusti 10 mwaka huu majira ya saa 8:00 mchana na ambapo tembo hao
walisababisha kifo cha Veronica John (44) na kumjeruhi vibaya Stiven Shirima.
Boaz alisema marehemu alikuwa shambani akiwa
anajishughulisha na shughuli za kilimo ambapo tembo hao walimkanyagakanyaga
sehemu mbalimbali za mwili pamoja na
kuchumwa na pembe mbavuni upande wa kushoto.
Kamanda huyo alisema hali hiyo ilimfanya avuje damu nyingi hali iliyopelekea kupoteza
uhai na kwamba majeruhi wanapatiwa matibabu katika hospitali ya huruma huku
mwili wa marehemu ukiwa umehifadhia katika hospitali hiyo.
EmoticonEmoticon