sumbawanga |
Na Edwin Moshi.
Sumbawanga, RUKWA..
Mkazi wa kijiji cha Ulumi tarafa ya mwimbi wilayani
sumbawanga katika mkoani Rukwa Issack Lunguya (40) amehukumiwa kifungo cha
miaka 2 jela ,sanjari na kulipa faini ya 2,000,000/=kwa kosa la kujalibu
kumuuza mtoto wa jirani yake ili akatumikishwe kazi za ndani bila ridhaa.
Mwandishi wa habari hizi anaripoti kutoka
Sumbawanga kuwa ,Adhabu hiyo imetolewa katika mahakama ya Hakimu mkazi mjini
Sumbawanga wakati hakimu wa mahakamani ya hakimu mkazi Rozalia Mugissa baada ya
kuridhishwa na ushaidi wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo iliyoongozwa na
mwendesha mashtaka wa polisi Assistant Ispector Emmanuel Shani.
Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha mashtaka Mkaguzi
Msaidizi wa Polisi
kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo 07,08 mwaka huu,amapo
alikamatwa febr 21/2012 saa nne asubuhi huko ulumi alipokuwa katika harakati za
kumuuza mtoto huyo mwenye umri(14)kwa mfanyabiashara mmoja ili asafirishwe
kupelekwa mjini sumbawanga tayari kwa kwenda kufanya kazi za ndani.
Shani aliendelea kuileza mahakama hiyo mbele ya Hakimi Mkazi
wa Rosaria Mugissa kuwa siku ya tukio mshtakiwa, kabla ya hapo kulikuwa na
taarifa za siri kwamba mtuhumiwa, alikuwa akitafuta mteja wa kumuuzia mtoto
huyo ambaye ni jirani yake ile hali ni yatima kwa kiasi cha 2,000,000, alimvizia
binti huyo akitoka nje kwenda kujisaidia.
Aliendelea kuielezea mahaka hiyo kuwa uliandaliwa mtego kwa
kumtumia mtendaji wa kijiji hicho na hatimaye mwanaume huyo akanaswa akiwa
amemleta mtoto huyo sokoni huku akiwa anamdanganya kuwa anaenda kumtafutia kazi
nzuri ya kuuza duka.
Hakimu Mugissa alisema kuwa ameridhishwa pasipo kuwa na
shaka kwani ushahidi,watu watatu akiwamo binti huyo aliyetaka kuuzwa ambaye
aliielezea mahakama kuwa yeye ni yatima na hasomi shule kutokana na kukosa mtu
wa kumsomesha ikiwa kwamba siku ya tukio alirubuniwa na jirani huyo.
Alisema kutokana na shida alizokuwa nazo alilazimika
kuongozana na jirani yake,mpaka walipofika kwenye nyumba moja pale ulumi
alielezwa abakie nje kwanza huku yeye aingie ndani,baada ya muda mfupi alishtukia
mwenyeji wake anakamatwa akiwa anapokea fedha.
Akitoa hukumu hiyo Mugissa alisema kutokana na upande wa
mashtaka umethibitishwa pasipo kuacha shaka kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo
kwa vile vitendo vya wananchi kuwauza,pamoja na kuwasafirisha watoto kwa lengo
la kuwatumikisha kazi ngumu vimeshamiri,ile hali akititoa adhabu hiyo ili iwe
fundisho kwa mshtakiwa mwenyewe na wengine wenye tabia kama hizo tayari ameanza
kutumikia kifungo kwa kukosa fedha za kulipa faini.
EmoticonEmoticon