IGP SAID MWEMA |
TARIME, MARA
MTOTO mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja ameuwawa baada ya
kupigwa fimbo kichwani na baba yake mzazi Migengo Mseti (68) Mkazi wa Kijiji
cha Nyakunguru kata ya Kibasuka Wilayani Tarime.
Kamanda wa Mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo nakwamba lilitokea Agosti 8 majira ya saa
10.30 jioni kitongoji cha Turuturu kijiji cha Nyakunguru ambapo mtoto aitwaye
Buyuri Mseti aliuwawa.
Kamanda Kamugisha alisema kupigwa kwa mtoto huyo kulitokana
na sababu za ugomvi kati ya baba na mama yake Magreti wakati baba huyo akimpiga
mke wake alikuwa amebeba mtoto mgongoni na kwamba wakati baba akijaribu kumpiga
mke wake kwa fimbo mama huyo alikwepa fimbo na ndipo ilipompata mtoto Kichwani
na kumsababishia kifo papo hapo.
Kamugisha aliongeza kuwa mwili wa marehemu umefanyiwa
uchunguzi tayali kwa mazishi nakwamba mtuhumiwa amekamatwa na yuko chini ya
ulinzi na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.
EmoticonEmoticon