Na Black Touchez/daily mail
WATAFITI kutoka katika Kitengo cha PSYCHIATRY,
kilichoko katika Chuo cha Cambridge, wamedai kuwa Mashairi ya Muziki wa Hip Hop
yanayozungumzia Wanawake , magari na hata Maisha Mazuri, yanaleta matumaini
hasa kwa waskilizaji na mashabiki mbali mbali ambao wanafuatilia sana muziki
huo.
Mmoja wa Timu hiyo ya Utafiti, Dr. Becky Inkster
, amedai kuwa waliweza kubaini hilo katika Clinic yake ambayo muda mwingi
wamekuwa makini sana kufuatilia project yao ya HIP-HOP PSYC, ambapo wamegundua
kitu hicho kwa usahihi
Idha Mtafiti huyo amedai kuwa, Nyimbo ambazo
zinazungumzia Madawa ya Kulevya, maisha ya Jela, Uvutaji bangi na Matatizo
mengine ya Kihuni, yamekuwa yakiwaathiri vibaya watu tofauti tofauti hasa
vijana , na hata kupelekea wao kukata tamaa
Lakini Pia ameongeza kuwa, Nyimbo za magari na
maisha Fulani hivi ya thamani ama ufahali, yamekuwa yakiwapa matumaini sana
wadau na hata wapenzi wa muziki huo
Dr Inkster amemalizia kwa kusema kuwa, hivi sasa
wanahitaji kusambaza matunda ya Project ya HIP HOP PSYC katika maene o mbali
mbali ikiwemo kutoa Elimu katika MAGEREZA MBALI MBALI, SHULE,na HOSTELS mbali
mbali za wanafunzi.
EmoticonEmoticon