MAREHEMU GEEZ MABOVU: rapa huyo aliondoka Dar
kwenda Iringa akiwa kwenye hali ambayo sio nzuri kiafya.
|
Frank M. Joachim
SIMANZI Nyingine imeivaa Tasnia ya Muziki wa
Kizazi Kipya-HIP HOP baada ya kumpoteza Msanii aliyekuwa akifanya Harakati zake
kwa muda Mrefu Sasa
Ahmed Ally Upete 'Geez Mabovu' amefariki dunia
jana usiku akiwa mkoani Iringa alikokwenda wiki mbili zilizopita akitokea
jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa bwana Dennis ambaye alikuwa mtu wa
karibu wa Geez Mabovu amethibitisha kuhusu kifo hicho na kusema rapa huyo
aliondoka Dar kwenda Iringa akiwa kwenye hali ambayo sio nzuri kiafya. Marehemu
Geez Mabovu anatarajiwa kuzikwa leo Novemba 13, 2014.
YOUNG KILLER: Ameahirisha Kauchia Video ya “13”
kutokana na Kifo cha GEEZ MABOVU.
|
·
Young
Killer Ameahirisha Kuachia Video Yake Ya 13
Kutokana na Kifo Hicho, Wasanii kadhaa wameweza
kutoa Salamu zao za rambi Rambi, nab ado watu tofauti hasa wadau wa Muziki wa
Kizazi Kipya wakizidi kutoa Salam zao pia Za Rambi rambi kwa Familia.
Kwa Upande wake Young Killer “Msodoki” ameamua
kuahirisha Kuachia rasmi leo Video yake 13, aliyomshirikisha Fid Q pamoja na
Belle
9
WEUSI: KUSEMA UKWELI HATUTOWEZA KUFANYA SHOW YA
MBEYA…NI KWA SABABU GEEZ NI MSHIKAJI WETU, HE IS PART OF THE FAMILY.FOR THE
LOVE OF HIP HOP AND RESPECT, HATUTAWEZA KUFANYA”
|
·
Weusi
Waahirisha Show Yao “Funga Mwaka” Iliyokuwa Ifanyike Mbeya
SHOW ya Funga Mwaka ilikuwa ifanyike Ijumaa hii
kule Jijini Mbeya, lakini Joh makini akiwakilisha Familia ya WEUSI, amesema
kuwa, hawatoweza kufanya Tena Show hiyo Siku husika, kutokana na Kifo cha GEEZ
Hapa tunamnukuu JOH MAKINI:
“KUSEMA
UKWELI HATUTOWEZA KUFANYA SHOW YA MBEYA…NI KWA SABABU GEEZ NI MSHIKAJI WETU, HE
IS PART OF THE FAMILY.FOR THE LOVE OF HIP HOP AND RESPECT, HATUTAWEZA KUFANYA”
EmoticonEmoticon