REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

UPDATE: ALIYEMSHTAKI JUSTIN BIEBER, YAMEMGEUKIA:

6:39:00 AM

LOS ANGELS, Marekani

UKiskia Mtu anakwambia Tit For Tat, basi Uje kuna Kitu kikubwa sana Kinachokuja..Sikia Hii, Baada ya TTM Jana kukupa Data kuwa JUSTIN BIEBER anashitakiwa kwa kosa la Unyang’anyi na Mwanamke Mmoja hivi, hatimaye Kibao kimegeuzwa hasa katika Suala Zima La Upelelezi.

Mbwadidi limekuja Sehemu Moja Tu, ambayo Ni Ushahidi wa Mfanyakazi mmoja kutoka katika Jumba hilo la Biashara la THE SHERMAN OAKS CASTLE PARK kudai kuwa aliona Tukio zima lililotokea baina ya Justin Bieber na Mwanamke huyo aliyekuwa akijaribu kumpiga Picha Bila Ridhaa yake.

Mfanyakazi huyo ambayye jina lake halikupatikana fasta, amedai kuwa, Mwanamke huyo aliyefungua mashtaka, Ndiye alikuwa Mkorofi, mtovu wa Nidhamu, na hata kutokusikiliza kile alichoambiwa na Walinzi, hasa kutokumpiga Picha Bwana Mdogo Bieber.

Pia Mfanyakazi huyo alizidi kusisitiza kuwa, Justin Bieber hakujaribu Kumuibia N’GWANIKE HUYO a.k.a Mwanamke Huyo Simu yake, na wala hakutaka kumjeruhi na hata Kumdhalilisha.

Tofauti na hayo, kwa Mujibu wa info za Rafiki wa karibu wa The Majanga Bwaaaay, inasemekana kuwa, Bieber alipata hasira baada ya Kuona Kila Mara Flash zinamuandama, hasa ikiwa Ni Camera ya Huyo mwanamke.


Hata Hivyo Mfanyakazi wa Jengo hilo, amedai kuwa, ili kuthibitisha Tukio Hilo, Uchunguzi ungefanyika katika kamera za Ulinzi wa Jengo Hilo, ingawa kuna Uwezekano ikawa ngumu kidogo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER