UNAWEZA Kujiuliza huyo mtoto alimpata wapi,
lakini Swali hilo wala sina jibu, Ila Mtonyo uko hivi…
“MNAIJERIA” aliyelifanyia haki Vilivyo Kwaju
lake la KUCHI KUCHI, JODIE ODIETE amevunjia ukimya swali aliloulizakuhusu Suala
la mapenzi ama Ndoa kiujumla, wakati akipiga Moja ya Interview Nchini Nigeria.
Katika maelezo yake baada ya kuulizwa
analichukuliaje suala la mapenzi Kiujumla, Jodie alikiri Kuwa kwa upande wake
haoni kitu chochote cha Muhimu katika Suala Hilo, maana hana Uzoefu:
“Binafsi, silichukulii kiulazima kiasi hicho
maana SIJAOLEWA, na haya ni mawazo yangu wala simgusi Mtu yeyote. Siwezi kuwa
na Mtizamo wowote katika mapenzi kwa sababu kwanza sina UZOEFU na Kitu
kinachoitwa mapenzi. Kwa maana hiyo, kufanya mapenzi,ama mapenzi kiujumla, si
lolote si chochote kwangu, na ndiyo maana siwezi kujihusisha na mahusiano ya
kimapenzi kwa sababu hiyo.” Alisema Jodie..
Tofauti Na hilo, Bado Jodie alizidi “Kumiminika”
baada ya kuulizwa kuhusu Mwanamme ambaye anamtamani na hata kumfikiri kuwa nae
maishani, :
“Ninahitaji Mwanaume ambaye ni Rafiki yangu,
ambaye atakuwepo kwa ajili yangu muda wowote. Ni ngumu sana kumpata mwanaume wa
aina hiyo katika Dunia hii hatarishi. Hivyo kwa upande wangu ninahitaji
Mwanaume rafiki ambaye kiujumla atajitolea kwa ajili yangu. Siwezi kusema
anatakiwa awe Mrefu, mweusi, Mfupi, mnene, na mengineyo, bali ninahitaji
Mwanaume ambaye ni rafiki wa Dhati”
EmoticonEmoticon