REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MWANZA IS THE BEST: MUZIKI WA MWANZA TUMEUSUSA, LAKINI MABINTI HAWA WANAHITAJI SUPPORT KATIKA AINA YA MUZIKI WANAOFANYA (R&B na ZOUK)

4:38:00 AM

Nimebahatika kusikia Nyimbo tofauti sana za wasanii wengi wa kike kutoka jijini Mwanza. Tunashukuru wengine walitangulia katika mafanikio huku wakiibeba Heshima ya jiji Hili na Kuifikisha Sehemu Nzuri. Naweza kusema Ahsanteni sana.

Lakini hivi sasa Muziki umekuwa sana, na Vizazi vipya zinazidi Kuusukuma mpaka kuufikisha hapa ulipo.

Pasipo Kificho, Muziki wa Mwanza ni Mzuri sana, na kwa mtu yeyote anayeishi Mwanza, hakika hawezi kupingana na Hilo. Lakini kumekuwa na Changamoto kubwa sana ambayo inaukabili Muziki huu, na hata kufikia hatua ya kujenga “Ukuta” mkubwa baina ya mafanikio haya ya Muziki wa jiji hili, pamoja na soko kiujumla.

WAKAZI WA MWANZA wamekuwa ni sehemu kubwa ya kukwamisha maendeleo ya Muziki wa jiji hili tofauti na ilivyo katika JIJI la ARUSHA. Kuanzia kuusikiliza, kuufuatilia, kuusambaza na hata kuuandalia matamasha mbali mbali, vitu hivi vimekuwa ni historia kwa wasanii wa Mwanza na kazi zao. Ni sehemu chache sana hasa za Ndani, ambazo zimekuwa zikupa “Kik” Muziki huu, Mfano Mzuri ni UKEREWE.

Tofauti na Hilo, WADAU WA MUZIKI “FEKI” wamekuwa Wengi sana. Tukubali tukatae, Suala la “Menejimenti” Limekuwa ni tatizo kwa Mwanza Tu, bali hata Nchi nzima. Tumekuwa tukisikia wasanii kadhaa wakubwa wakilalamika Utapeli na ujinga unaofanywa na Wanaojiita mameneja, lakini Mwisho wa siku hakuna kinachofanyika katika kufaidika na Muziki wao. Tunakubali, ni vema kujitolea kumsaidia Msanii kuanzi kumsimamia katika kazi zake, lakini ukweli ni kwamba, mameneja hawa pamoja na Wadau wengine “feki” wanaongeza kila siku, na wanawatumia sana wasanii hasa hawa chipukizi ama wenye hamu ya kufanikisha kazi zao, kujinufaisha wao wenyewe.

UDHAMINI hasa katika matamasha, umekuwa kikwazo pia. Iko hivi, katika jiji la Mwanza, ukiandaa Tamasha (Shows, Events) ambazo zitawahusisha wasanii wa Mwanza tu, halafu ukaombe udhamini, Hesabu maumivu kabisa. Lakini ukiandaa tamasha ambalo litamuhusisha Diamond, Madee, Chege, na wengineo wengi tu, wenye majina, basi hapo utawapata unaowataka. Undhani hii itaufanya Muziki wa Mwanza ufikie pale unapotakiwa Kufika?

EMMY SANGO NA HONEYA…WANAHITAJI KUFIKA PAZURI.

  •   EMMY SANGO

Usinibanie Ndiyo Track ambayo Kiujumla ilimtambulisha Emmy katika Muziki wa Zouk hapa Mwanza, na hata kwingineko. Uwezo wake ulidhihirishwa na Track yake ya Pili inayofahamika kwa Jina La RADIO PRESENTER.
Kiufupi, Uwezo wake uko Vizuri sana, tangia nimeanza kumsikiliza, kuurudia mara kadhaa, kuwahusisha wenzangu, hakika anaweza kushindana na Wasnii wa kike kama akina linah, na Wengineo.


  •  HONEYA.

Infact, UWE WANGU, ndiyo Track yake ya Kwanza kaisa kurecord na hata Kuiachia. Ukiisikiliza kwa Umakini, unabaini kabisa kuwa bnti huyu anaimba kwa hisia sana, na anajua kipi ambacho anatakiwa kufanya katika “TOPIC” ya Wimbo anaouimba.
Sauti yake na mpangilio wa uimbaji wake, lazima utadhani amepitia “Training “ yoyote ya sauti, lakini nilipozungumza naye alisema hajawahi kupitia Training College yoyote hasa ya Sauti.
KWA MANTIKI HIYO, hebu tutafanye kitu kimoja. Sisi wasikilizaji, Wadau wa Muziki, watangazaji wa Redio mbali mbali kama Mie, Bloggers wote ambao tumejitambulisha ku-support Muziki wa Tanzania, tuwasikilize mabinti hawa, na tuwasukume. Ingawa ni kweli mapungufu yapo, lakini kupitia wewe, kila kitu kitakuwa ni funzo tosha kwao, na hatua nyingine nzuri zaidi kwao.

Mwanza is the Best


PATA NAFASI YA KUZISIKILIZA NYIMBO ZAO KWA UMAKINI

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER