BBC & DAILY MAIL
Kundi la wanamgambo wa kiislamu la
Islamic state limetoa ukanda wa video unaoonyesha mateka Alan Henning raia wa
Uingereza akikatwa kichwa.
Henning mwenye umri wa miaka 47 ambaye ni dereva
wa texi kutoka kaskazini mwa Uingereza alitekwa nyara mwezi Disemba mwaka uliopita
alipokuwa akilifanyia kazi shirika moja la kutoa huduma za misaada kwa
wakimbizi nchini Syria
.
Kundi la Islamic State ambalo limechukua
udhibiti kwenye maeneo ya mpaka kati ya Syria na Iraq tayari lishawaua
waandishi wa habari raia wa Marekani James Foley na Steven Sotlof pamoja na
mfanyikazi wa kutoa huduma za misaada kutoka Scotland David Haines.
Mapema babake John Cantlie raia wa Uingereza
ambaye anashikiliwa mateka na wanamgambo wa Islamic State aliomba kuachiliwa
kwa mwanawe.
EmoticonEmoticon