TIMES FM 10.5MHz, Dar Es Salaam
Mwimbaji wa Bongo
Flava kutoka Morogoro, Belle 9 hafikirii kufanya collabo na Diamond Platinumz
hivi karibuni kwa kuwa bado haoni chemistry (muendano sawa) kati yao.
Akiongea katika
Exclusive Friday ya kipindi cha Sunrise cha 100.5 Times Fm, Belle 9 amesema
haoni kama kuna chemistry kati yake na mwimbaji huyo ingawa haweki mipaka ya
collabo kati yao, ikitokea wamepata kitu wanaweza kufanya.
“Kama ikitokea nina
wimbo ambao yeye anaweza kuplay part yake vizuri tunaweza tukafanya. Ikitokea
mimi nimeandika wimbo ambao nahisi kabisa yeye akikaa atafit tunaweza
tukafanya. Lakini sio chemistry hapo kwanza.” Belle 9 ameiambia Sunrise ya
100.5 Times Fm.
Mwimbaji huyo amesema
hivi sasa anafikiria kufanya kazi na mzee Zahir Zorro au Banza Stone kwa ajili
ya kupata kitu cha kipekee.
“Hawa vijana wanaimba
vizuri. Kiwango kipo, sijasema sioni… lakini the same. Mimi ninahitaji kitu
unique kwa sababu nahisi kwa kumshirikisha Zahir au Banza Stone hivi…yaani watu
ambao mimi naweza kuchukua kitu pale. Kuna watu wengi ambao naweza kujifunza
vitu vingi.” Belle 9 amefafanua.
Hata hivyo, amesema
wasanii wapya wa kizazi kipya wanafanya vizuri sana pia na akawataja wengi
aliowashirikisha kwenye nyimbo zao kuonesha jinsi anavyowakubali.
EmoticonEmoticon