REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MKUU WA MKOA: HAKUNA EBOLA MWANZA

2:06:00 AM

Mkuu Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akitoa taarifa ya mkoa kuhusu kanusho la kuwepo kwa mgonjwa wa Ebola wilayani Sengerema


Na G.SENGO BLOG, Mwanza
TAARIFA zinazosambazwa kuwa kuna mgonjwa wa Ebola kagundulika wilayani Sengerema mkoani Mwanza, si za kweli.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo jijini Mwanza, Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Dr. Kengia amesema utafiti wa awali kabla ya majibu kamili ya vipimo unatosha kujidhihirisha kuwa mgonjwa aliyedaiwa kufariki dunia hivi majuzi Salome Richard (17) siyo kweli kwamba amefariki kwa Ebola.

Hata hivyo kulikuwa na uchukuaji wa vipimo vya awali ambapo, Majibu ya Vipimo vya awali yamepatikana tarehe 19/10/2014 saa 3:00 asubuhi

VIPIMO WALIVYOPIMA 
1. Dengue fever
2. Chikungunya Virus
Majibu ya vipimo hivyo walionekana ni Hasi (Negative)

VIPIMO VINGINE VINAVYOENDELEA 
(1) Liver function - kuangalia kama ini la mgonjwa ambaye ni marehemu lilikuwa kinafanya kazi vizuri au la.
(2) Bilirubin kuangalia kiwango cha protein kwenye ini kama kilikuwa sahihi au kimeongezeka.
Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Dr. Kengia.

Taratibu zinaendelea kati ya Mkuu wa Maabara ya Taifa na Wizara ya Afya kuhusu sampuli hii kupelekwa Mbeya au jijini Nairobi nchini Kenya kwaajili ya uchunguzi wa virusi ya Ebola au Marbug.

Awali kutokana na hofu ya ugonjwa huo huku taarifa zisizo rasmi zikizidi kusambazwa kwa njia ya mitandao ya simu na internet wananchi wa wilaya ya Sengerema na vijiji vya karibu walihaha katika vyombo vya usafiri husussani daladala wakikataa kugusana kwa kuwa Ebola imeingia Mwanza, huku wafanyakazi na wafanyabiashara wanaoishi mkoani Mwanza na kufanya shughuli zao wilayani Sengerema wakiahirisha kuelekea wilayani humo kutokana na vitisho vya taarifa walizopata.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER