Na ELIZABETH JOHN, Dar Es Salaam
MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya
nchini, Haruna Kahena ‘Inspector Haroun’ au ‘Babu’ anatarajiwa kufanya shoo ya
kuadhimisha miaka kumi ya ndoa yake, itakayofanyika Octoba 25 katika ukumbi wa
Mpoafrika Devis Corner, Temeke Dar es Salaam.
Kiingilio katika shoo hiyo iliyopewa
jina la ‘Usiku wa Wakongwe’ kitakuwa sh 5,000 na itaanza saa mbili usiku na
kuendelea ambapo atasindikizwa na wakongwe kibao.
Akizungumza jijini
Dar es Salaam jana, Inspector alisema kuwa, anaomba mashabiki wa muziki wake
wamwagike kwa wingi katika ukumbi huo kwa lengo la kupata burudani ilikwenda
shule.
Alisema atasindikizwa na Luten
Karama, TID Mnyama, Scorpion Giirlz (Isabela), LWP & Mabaga Flesh, Young
Tuso & Drama Boy na Kimbiza Dj’s.
Inspector alisema kuwa siku hiyo
atafanya shoo kubwa ambayo hajafanya kwa muda mrefu hivyo wapenzi wa kazi zake
wanatakiwa kumwagika kwa wingi.
Mkongwe huyo alishawahi kutamba na
ngoma zake kama Asali wa Moyo, Sharubu za Babu, Mungu ndio anapanga na nyingine
nyingi ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.
EmoticonEmoticon