HAKUNA Mtu ambaye
huwa anapingana na makali ya Sheria hasa ukizingatia marungu makali ambayo
unaweza ukakutana nayo hapo baada ya kujifanya kiburi cha Wenye Viburi.
THIS time Sifa kali zimeshushwa ka
Rapper Mkorofi na Mwenye Kiburi, KANYE WEST, baada ya kufanyiwa Tasmini katika
Adhabu aliyopewa na mahakama, ya Kifungo cha Nje, pamoja na Kufanya Shughuli za
Kijamii
Kwa Mujibu wa Info kutoka kwa Hakimu
pamoja na Mwanasheria wa rapper Huyo Siku ya jana, Tasmini imedai kuwa, Rapper
Kanye West anafanya Vema sana katika Shughuli za Kijamii, pamoja na Kujiweka
Mbali na matatizo ambayo yanaweza kumsababishia hasira na hata kukiuka
Makubaliano ya Adhabu yake
Moja kati ya Shghuli za Kijamii
ambazo ameshafanya na kuvutia Wengi, ni baada ya Kanye kuhudhuria katika
Mahafali Moja hivi ya wanafunzi wa Chuo Kinachojihusisha na Masuala ya Fashion,
na kuzungumza nao kuhusu uzoefu alio nao katika Masuala hayo, ikiwa ni
kuwaongezea elimu.
KANYE WEST ambaye ni Baba wa Mtoto
North West mwenye Mwaka 1 na Mwezi Mmoja, alikutana na Ahdabu kali ikiwemo ya
kuwa Chini ya Uangalizi wa Miaka Miwili katika Suala la Kupiga watu, hasa
Waandishi wa habari, pamoja na adhabu ya kufanya Shughuli za kijamii ambapo
ameshamaliza masaa 250, sanjari na kuhudhuria mafunzo ya kujua namna ya
kucontrol Hasira zake, kwa muda wa masaa 24.
EmoticonEmoticon