KUNA uwezekano Mkubwa kabisa, kuna wengi
wameshalizwa Mikwanja ya Kutosha pamoja na Vitu kadhaa, kutoka kwa Mtu ambaye
ametengeneza account Feki ya Mshiriki wa BBA The Chase akiwakilisha jiji la
Nchi ya kenya, HUDDAH MONROE.
Kupitia account yake ya Twitter na Instagram,
Bibie huyo ambaye huwa anashikilia Vichwa vya habari kwa Kucharaza Picha za
utupu, amedai kuwa, Hivi sasa hana account yoyote ya facebook, wala Page, hivyo
unaweza kutafsiri kuwa, this mamito hayupo kabisa katika Mtandao wa Facebook.
Huddah ambaye pia aliwahi kukunjuka na
Rapcellency CMB Prezzo, ameongeza kuwa, wale wote ambao wanajifanya ni wazuri
wa kutumia vibaya jina lake hasa kutapeli kupitia Mtandao huo wa facebook, wanatakiwa kuacha mara moja, sababu
wanamkosea na hata kumtaftia matatizo.
Tofauti na hayo, TTM imegundua kuwa, Huddah
hapendi mtu yoyote tumie jina lake katika zoezi la utapeli ambalo linaendelea
mpaka hivi sasa, na iwapo atakuja kumnyaka, basi atamfanyia kitu ambayo
itasimuliwa kwa kila kizazi.
EmoticonEmoticon