IKIWA takriban
ni miezi minne kasoro tangu gwiji wa muziki Muhidin Mohamed Gurumo ‘Maalim
Gurumo’ aiage dunia, gari aina ya Toyota Fun Cargo alilopewa kama zawadi na
staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdu ‘Diamond’ limedaiwa kupigwa bei.
Kwa Mujibu wa info ambazoTTM,
inasemekana kuwa, chanzo cha Ndinga Hiyo kuingizwa Sokoni, ni baada ya kutokea
Mvutano baina ya baadhi ya Ndugu wa Mke wa Marehemu, PILI NASSORO, ambao
walifikia mpaka hatua ya Kufikishana katika Kituo cha Polisi.
Taarifa zaidi zimezidi kumiminika
kuwa, kuna watoto wa Marehemu ambao walitaka kulipiga Bei gari hilo , Muda
Mchache tu baada ya kumalizika kwa Masiba wa Marehemu Gurumo, lakini utata
ulizidi kuwa mkubwa zaidi baada ya Mke huyo wa marehemu kutia Ngumu, huku
akisemekana kuwa, Marehemu aliacha Wosia kuwa, pindi atakapofariki, Kadi ya
Mkoko huo ikabidhiwe kwa Mkewe, maana kabla hajafariki alishajua tamaa ya
baadhi ya Ndugu yake
Hata hivyo inasemekana kuwa, kwa
Kulitambua hilo, Marehemu alimkabidhi
Kadi ya Gari, Meneja wa Diamond Platnumz, HAMIS TALE “Babu Tale” ili
amkabidhi Mkewe (Bi Pili Nassoro) pindi atakapofariki.
Babu tale aliposakuliwa kunako Simu
ili aseme hayo, alithibitisha kuwa ni Kweli Kadi ya gari la Marehemu Gurumo
anayo, na alishapewa maagizo na Mke wa marehemu kuwa liwekwe Sokoni, hivyo
Yeyote mwenye kutaka kulinunua, basi milango iko Byee
Diamond alimkabidhi marehemu gari
hilo Agosti, mwaka jana katika Ukumbi wa Serena, Posta jijini Dar baada ya
kuguswa na mchango mkubwa alioutoa Gurumo katika tasnia ya muziki nchini.
EmoticonEmoticon