LEO Ni siku
ambayo another Mbwadidi linashuka kunako Music Industry hapa Bongo, huku
ikithibitika kabisa kuwa, Nay na Stamina Walipeana makali katika Track ambayo
wawili hao wamehusika.
Kwa mujibu wa maelezo ya Stamina
ambaye ndiye mmiliki wa Track hiyo, amedai kuwa Mkwaju huo ambao leo ndo
unaingia sokoni, utazua utata mkubwa sana kwenye game la muziki hapa Home,
ukizingatia wawili hao wamechanana kiukweli.
Aidha Stamina ameongeza kuwa, Track
hiyo ni ya majibishano, ambapo Nay wa Mitego ameact kama Msanii ambaye alikuwa
anafanya Hip Hop lakini kwa sababu yeye amejikita zaidi kwenye kusaka hela,
basi hivi sasa kaisaliti Hip Hop, huku Stamina “Shorobwenzi” Himself amesimama
kunako Hip Hop ambayo yuko nayo mpaka Hivi sasa.
Pia kwa mujibu wa majibishano hayo,
basi wawili hao wanatoa taarifa ama details za aina ya Muziki wanaoufanya, kitu
kinachokamilisha jina la Track hiyo HUKO KWENU VIPI.
Rapper huyo amesema kwamba, wameamua
kuiachia kwa haraka ngoma hiyo iliyofanyika siku tatu zilizopita katika studio
za MR. T-TOUCHEZ, kwa sababu vitu walivyoviongea ni vitu vya muda huu kwa hiyo
hawataki kukawia kwa sababu mambo yanaweza kubadilika.
STAMINA amemalizia kwa kusema kuwa,
kuwa katika ngoma hiyo Nay amefanya ubabe wa maneno bila kuogopa kutaja majina
ya watu na kwamba hata yeye (Stamina) amefanya hivyo kwa kuwa makubaliano yao
yalikuwa kuchanana bila kuogopa.
EmoticonEmoticon