(C) Mbeya Yetu |
MBEYA, Tanzania
WIMBI la wanawake mkoani Mbeya kujifungua watoto
na kisha kuwatupa na wengine kutoa mimba limezidi kushika kasi na kukithiri
baada ya vitendo hivyo kuripotiwa na vichanga kuokotwa kwenye mashimo na
mitoni.
Kukithiri kwa vitendo ni baada ya leo Wananchi
wa Mtaa wa Mwambenja kata ya Iganzo jijini Mbeya kugundua kutupwa kwa mtoto
anayesemekana kuwa na umri usiozidi siku moja jinsia ya kike katika shimo la
choo kisichotumika.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Mtaa huo,
aliyefahamika kwa jina la Lukasi Mwakalonge, alisema alipewa taarifa na
wananchi wake mchana na kuambiwa kuna katoto kametupwa shimoni na bado ni
kazima hali iliyomlazimu kutoa taarifa katika Jeshi la Polisi.
Alisema baada ya kufika eneo la tukio na
kugundua kuwa mtoto bado yuko hai wakaamua kumtoa ndani ya shimo huku wakisubiri
jeshi la polisi kwa ajili ya hatua zaidi lakini akawa amepoteza maisha muda
mfupi baada ya kutolewa ndani ya shimo.
Hata hivyo jeshi la Polisi lilifika eneo
la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu, vitendo hivyo vya wanawake kutupa
watoto kabla na baada ya kujifungia bado vinazidi kutokea hapa nchini ingawa
hakuna takwimu sahihi za wanawake waliopatikana na hatia kwa makosa kama hayo.
NA MBEYA YETU
EmoticonEmoticon