Tasisi kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru)
mkoani Kilimanjaro, imewatia mbaroni wafakazi watatu na kuwachunguza
wawili wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), kwa kosa kuomba na kupokea
rushwa ya Sh. 400,000.
Wafanyakazi hao wanadaiwa kwenda nyumbani kwa
Baltaza Zafa Ally, mkazi wa Shant Town Manispaa ya Moshi, kwa malengo la kukata
umeme wa nyumba hiyo kwa madai kuwa alikuwa akidaiwa na shirika hilo.
Baada ya akufika nyumbani kwa mteja huyo, Wafanyakazi hao walikuta geti limefungwa ndipo walipoingia kwa kuruka ukuta wa geti na kuanza kukagua mita ya umeme na kudai kuwa mita hiyo imechezewa na kumtaka mteja huyo awalipwe Sh. million moja ili wasikate umeme.

Kwa Upande wake Baltaza amefafanua kuwa,
watuhumiwa hao walifika nyumbani kwake kwa kuruka ukuta na kuingia ndani na
kuanza kusoma mita, baada ya kumaliza kusoma miti hiyo ndipo walipomwambia kuwa
mita hiyo imeonekana kuchezewa na kisha kumwambia awape fedha ili wasikate
umeme.
EmoticonEmoticon