Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini, Kanda
ya Kaskazini wamethibitisha uwepo wa hazina ya madini ya dhahabu katika Mlima RANKIROGA
na Mto KARABALINE katika Kijiji cha Mgongo, Kata ya Samunge, Wilaya ya
Ngorongoro Mkoa wa Arusha.
Kamishna wa Madini Kanda ya Kaskazini, Alex
Magayane amesema kuwa Ofisi yake imefanya utafiti wa awali katika Kijiji cha MGONGO
na kubaini uwepo wa dhahabu hiyo.
Habari kutoka Samunge zinasema wachimbaji
wanazidi kumiminika kusaka madini hayo yaliyogundulika kuwapo kwenye mashamba
ya watu na maeneo ya kingo za mto huko Mgongo, kijiji kilichopo jirani na kwa
Mchungaji Mwasapile, maarufu kama Babu wa Loliondo.
EmoticonEmoticon