KAMA Unajiita “mtoto wa kishua” halafu
unategemea kila kitu kutoka kwa Dady na Momy, basi inabidi uwe na akili ya
Ziada, huenda wazazi wako wakawa na Akili kama za BILL GATES.
Katika mkutano wa TED 2014 huko Vancouver, Colombia,
Bilionea nayaeongoza kwa mkwanja ulimwenguni kote kupitia biashara yake ya
MICROSOFT, BILL GATES na mke wake MELINDA GATES, wamesema kuwa hawana Mpango wa
kuwatajirisha watoto wao watatu kupitia utajiri walio nao.
Ingawa ni Kweli wana utajiri wa kuwafanya watoto
wao kuwa mabilionea kwa kila Mmoja, Bill gates amesema kuwa kitu ambacho
wanadhani Ni kizuri na kina ubora, ni kuwapa uhuru watoto wao kujishughulisha
kwa bidii zote ili waweze kujivunia Nguvu na juhudi zao.
Pia katika ufafanuzi mwingine, Bill gates amedai
kuwa, Watu wasidhani kuwa watoto wao wamekulia katika maisha ya hali ya juu
sana huku wakipata matunzo ya Gharama kubwa, bali waliishi maisha ya Kawaida.
“Watoto Wetu wamelelewa na kukua katika
mazingira ya kawaida sana. Tuliishi katika nyumba ya hali ya kawaida ambayo
niliinunua Mwaka 1958. Tofauti na hayo, bado watoto wetu hawakupata nafasi ya
kupanda Ndege Kubwa za Binafsi. Walikuwa wakienda shuleni kwa Mabasi ya shule
ya kawaida, na walisoma Shule ambazo ni za umma, maana hata mama yao alisomea
huko huko”
Alisema Bill Gates
EmoticonEmoticon