MWANARIADHA Mlemavu, Oscar Pistorious ambaye
anakabiliwa na mashitaka ya Kumuua Mpenzi wake, mwanamitindo REEVA STEENKAMP,
ameamua kuiuza nyumba yake kubwa ya kifahari iliyoko katika mji wa Pretoria,
nchini Afrika ya Kusini.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mwanasheria wa familia
ya Pistorious, BRIAN WEBBER, amesema kuwa, awali Oscar Pistorious alikuwa
amepanga Kufunga nyumba hiyo na Kuiacha mpaka pale Maamui dhidi ya kesi yake
yatakapotolewa, lakini kulingana na kuongezeka kwa Gharama za uendeshaji wa
kesi yake,, imemlazimu kuipiga bei.
Pia Webber ameongeza kuwa, Pistorious hajawahi
kurudi tena katika Himaya yake hiyo tangia siku aliyompiga Risasi Mpenzi wake
huyo, na hana mpango wa Kurudi tena katika nyumba hiyo Mpaka hivi sasa..
Mjengo huo unauzwa kwa Kiasi Cha Dolari za
kimarekani 456,000, sawa na Shilingi za kitanzania 7,29,600,000.
Aidha baadhi ya wataalamu wa masuala mbali mbali
hasa ya kibiashara, wamedai kuwa kuna uwezekano nyumba hiyo ikachukua muda
mrefu kununuliwa, kutokana na tukio lilitokea ndani yake
Kesi ya Oscar Pistorious, itaendelea kusikilizwa
tena Kuanzia mwezi wa Nne, na huenda ikachukua muda zaidi, kutokana na ushahidi
kuzidi kutafutwa
EmoticonEmoticon