Baada ya Dogo Janja kuuomba msamaha kupitia
vyombo vya habari uongozi wa Tip Top Connection na Madee aliyemtoa Arusha, Boss
wa Tip Top Connection Babu Tale amemiminika kuwa kuwa anataka rapper huyo aseme
ukweli wa yote aliyoyasema awali baada ya kutoka Tip Top.
“Aongee ukweli tu haina shida, nimemsamehe yeye
ni Muislamu mwenzangu tumetumwa tusameheane, mimi nimeshamsamehe ila
nimezungukwa na mashabiki ambao wakati yeye ananitukana kuna mashabiki ambao
walikuwa upande wangu ingawa walikuwa hawajui kama dogo alikuwa anaongea ukweli
au uongo.” Amesema Babu Tale.
Babu Tale ameweka wazi vipengele ambavyo
anataka Dogo Janja aviweke sawa.
“Dogo anatakiwa aseme kama kweli aliibiwa, kama
kweli alidhurumiwa na kama kweli hajawahi kuishi nyumbani kwa Madee. Anatakiwa
aongee dhahiri asifiche, aongee tu ukweli.” Babu Tale ameeleza.
Pia Amegusia pia tukio ambalo lilimsikitisha zaidi
wakati Dogo Janja anafanya kazi akiwa chini ya menejimenti ya Mtanashati
Entertainment.
“Siku zote kwenye ukweli uongo hujitenga, wakati
yuko South Africa alipost picha ‘ningekuwa Tip Top nisingefika huku’.
Nilishangaa heeh huyu kutoka huko kijijini kwao alifanyaje hadi kufika hapa!
Wazazi wake nao wakawa wamekubali uongo wa
mtoto wao wakaanza kutuongelea na sisi maneno ambayo ni uongo. Ulikuwa uongo wa
watoto halafu bado wao wanakandamiza uongo zaidi ya uongo. Kwa kuwa ni mtoto
kuna wazazi ambao walisimama nyuma yake ambao nao walikuwa wanasapoti. Aongee
ukweli mimi ntamsaidia.” Babu Tale ameeleza.
Babu Tale ameeleza kuwa Dogo Janja ameshamtafuta
kwa njia ya simu lakini amemwambia ujumbe ule ule kuwa awaambie ukweli
watanzania.
Kwa upande wa dogo janja, ameongea amesisitiza kuwa. binafsi hakutaka kuizungumzia kwa undani kauli ya Babu Tale, zaidi alieleza
kuwa alichokifanya kuomba msamaha alimaanisha kuwa alikuwa amekosea na hakuna
aliyemsukuma kufanya hivyo.
“Mimi nimeomba msamaha kwa kuwa nataka kuweka
mambo sawa na kumaliza tofauti na uongozi wangu wa zamani. Hivyo tu.
Wakinikaribisha Tip Top itakuwa poa tu pia…fresh.”
EmoticonEmoticon