NYOTA NDOGO ameshindwa kuvumilia kile ambacho
COLONEL MOUSTAPHA amekifanya kwa kupiga Picha za utupu na aliyekuwa mshiriki wa
BBA akiiwakilisha Nchi ya Kenya, HUDDAH MONROE.
Ili kudhihirisha kuwa amechukizwa na hilo suala,
Hatimaye Nyota Ndogo aliamua kuitisha Maandamano ya Wanawake ambao wamekwazwa
na Kitendo hicho, kushinikiza Jamaa huyo ambaye alikimbiza sana na Track yake
ya MTAANI.COM, ajirekebishe na hata Kuachana kabisa na Biashara Hiyo.
Katika Moja ya mabango ambayo yalionekana
kubebwa na Wanawake hao, ni pamoja na moja ambalo lilikuwa limeandikwa “COLONEL
MUSTAPHA HESHIMU WANAWAKE”
Aidha kwa upande wake Mustpha, alichukua uamuzi
sahihi wa Kuomba Msamaha kwa Huddah Monroe pamoja na wanawake ambao wamekerwa
na Kitendo hicho. Hapa namnukuu Mustapha akisema..
“Ninawaomba
msamaha kwa sababu ni lazima tu-respect wamama.”
EmoticonEmoticon