KAMA Utakuwa ni SUPPA FAN wa TTM, basi utakuwa
unakumbuka Vizuri kabisa kuwa tulikupa mtonyo kuhusiana na Ishu ya Naziz kuomba
Talaka kutoka kwa Mumewe.
Baada ya NAZIZI kuzungumza Mengi kuhusu Mchakato
huo, huku akithibitisha kuwa hivi sasa amebaki Singo na hakuna Tena Ndoa baina
ya wawili hao.
Kwa upande wake VINI LEOPOLD ambaye ndiye
alikuwa Mume wa nazizi, na wakafanikiwa kupata Mtoto mmoja wa kiume, amesema
kuwa kitendo cha kupeana talaka na Msanii huyo ambaye anaunda kundi la
NECESSARY NOISE na EAST AFRICAN BASHMENT CREW, hakijawafanya wao kuwa Maadui, na
bado wanawasiliana na Kuzungumza Vizuri.
Akizidi kufafanua kuhusu Hilo, Vini ameongeza
kuwa, Yeye na Nazizi ingawa kila mtu ana maisha yake hivi sasa, lakini bado ni
marafiki wazuri, sababu ukizingatia hata talaka waliyopeana, ilikuwa ni
makubaliano yao wawili na hakukuwa na Ugomvi
Aidha Vini ambaye alifunga Ndoa ya Siri na
Nazizi Mnamo Mwaka 2008, amesisitiza kuwa, Vyombo vya habari viache Kuandika
habari zisizo na ukweli kuhusu kuvunjika kwa Ndoa yao, kwani wana motto wao
Mmoja, na hatakiwi kukutana na Info hizo.
Katika Kumalizia, VINNY amewashauri mashabiki na
watu Mbali mbali, Kuupa Support Muziki wa Nazizi, huku wakiacha maisha yao
Binafsi yaende Sawa.
EmoticonEmoticon