BAADA ya kusambaa
kwa Info za UHAKIKA kuwa Mkali wa R&B na POP, Chris Brown atatupwa Jela kwa
Muda wa Mwezi Moja baada ya kukiuka Sheria za Rehab alikopelekwa kwa ajili ya
matibabu ya tatizo la Hasira, limezuka lingine tena ambalo ni muhimu
kulifahamu.
TTM tuliponyaka
hizo info, ilitubidi kufuatilia kiundani zaidi sababu ambayo ilimfanya Breezy
haswa, akafukuzwa Rehab, mpaka “Kuswekwa” Jela kwa Muda wa Mwezi Mmoja.
Kwa mujibu wa
Chanzo ambacho kimethibitisha kile ambacho tumekipata na tunatarajia
kukutaarifu, ni kwamba eti, Chris Brown alifikia mpaka hatua ya kufanya Mapenzi
na mmoja wa wanawake , wakiwa ndani ya Rehabu , kitu ambacho kilikuwa ni
ukikwaji wa sheria ya kukaa mbali na mwanamke yeyote akiwa hapo.
Aidha Chanzo
hicho kimeongeza kuwa, Kutokana na kosa hilo ,
Mkali huyo wa DEUCES alikiuka ,asharti ya Rehab na Mahakama, jambo ambalo
lilimfanya atimuliwe na Mahakama kumtupa Jela Mwezi Mmoja
EmoticonEmoticon