NAVicky Kombe, Morogoro
NYUMBA 25 na mashamba ya mazao ya chakula yanayokadiriwa
kufikia ekari 2908 katika kata ya Bwakira chini wilaya ya Morogoro, yamesombwa
na maji baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko.
Tukio hilo lililtokea Aprili 6 mwaka huo na kuvihusisha
vijiji vinne vya Bonye, Mbwade, Bwakira chini na Dakawa na hivyo kuwaacha
wakazi wake katika wakati mgumu.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Diwani wa
kata hiyo, Pessa Mohamed, alisema kuwa mafuriko hayo mbali ya kuharibu makazi
na mashamba ya mazao ya chakula, pia yameziacha familia 1598 zikiwa hazina
mahala pa kuishi.
Kwa mujibu wa diwani huyo, mazao yaliyoharibiwa na ekari
kwenye mabano kuwa ni mahindi (1158), mpunga (1143), ufuta (274), nyanya (3),
ufuta (27), alizeti (3) miwa (2) na nyanya (1).
Hata hivyo, alisema kuwa juhudi zinafanywa kuhakikisha
wakulima wanapata mbegu kwa kushirikiana na kitengo cha maafa katika wilaya
hiyo.
Alisema kutokana na mafuriko hayo, kata hiyo sasa inaweza
kukumbwa na njaa na hivyo ameiomba serikali na wadau mbalimbali kujitokeza
kusaidia mbegu za mahindi za muda mfupi kwa ajili ya kunusuru njaa katika kata
hiyo.
“Tunaomba wadau mbalimbali watusaidie mbegu za mahindi ya
muda mfupi kwanza kuliko kuleta chakula, hicho kitafuata baadaye,’’ alisema.
EmoticonEmoticon