Nasra Abdallah
SHULE za Sekondari nchini zimetakiwa kutuma maombi ya
ubunifu wowote wa kisayansi kabla ya Mei 31 mwaka huu, ili ziweze kuingizwa
katika mashindano ya Wanasayansi Chipukizi yanayotarajiwa kufanyika Septemba
mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Slaam jana,
Mkurugenzi wa Shirikisho la Wanasayansi Chipukizi, Dk. Kamugisha Gozibrt,
alisema katika mashindano hayo wanatarajia kupata shule 120 nchi nzima.
Alisema washindi katika shindano hilo watapata zawadi
mbalimbali ikiwemo, kompyuta pakato (laptop) na simu aina ya ipod kwa kila
mshindi, kompyuta kwa ajili ya shule wanakotoka washindi, sh milioni moja na
udhamini wa kwenda kusoma elimu ya juu katika chuo chochote nchini.
Dk. Gozibrt alisema mashindano hayo ambayo ni ya pili
kufanyika nchini yana lengo la kuwafanya wanafunzi kupenda masomo ya sayansi.
Alisema katika kuwawezesha wanafunzi hao kuja na mawazo
bora, wameanza kutoa semina kwa walimu wanaotoka baadhi ya shule za sekondari
ambao wataweza kushirikina kwa karibu na wanafunzi wao katika kufanikisha wazo
lao.
Akizungumzia changamoto, alisema kwa mwaka jana mashindano
hayo yalikuwa hayajajulikana hivyo ushiriki haukuwa mzuri, lakini kwa kwa sasa
kupitia vyombo vya habari wameanza kulielewa na tayari baadhi walishaanza
kutuma maombi.
EmoticonEmoticon