WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
HATIMAYE: CHAMELEONE AWAKUBALI HAWA...
Baada ya kufunika vilivyo kwa kutoa burudani ya nguvu katika
tamasha kubwa ambalo limefika huko nchini Uganda hivi karibuni msanii Jose
Chameleone amesema kuwa amewaomba mashabiki na wadau kuwapa sapoti wasanii wa
Goodlyfe, Moses Radio na Weasel TV.
Chameleone ambaye ni ndugu na Weasel TV alitumia nafasi hiyo
ya kuwaomba mashabiki katika tamasha hilo kutokana na kwamba wasanii hao
wamekuwa ni wenye mafanikio makubwa na kwamba katika wiki mbili zijazo
wanatarajia kufanya uzinduzi wa albamu yao waliyoibatiza jina ‘Obudde’.
Aidha Jose Chameleone alionyesha kuwa yeye ni gwiji na
mwenye kipaji katika tamasha lake la ‘Badilisha’ haswa alipoweza kuimba zaidi
ya nyimbo 40 ambapo pia aliziimba nyimbo za wasanii mbalimbali Afrika Mashariki
kama wimbo wa Kigeugeu wa Jaguar, Mukama wa Judith Babirye, Bread and Butter
kutoka kwao Moses Radio na Weasel TV, Kasepiki wa Bebe Cool na Wendi wa Bobi
Wine.
WASHAMBA:KWA WALE WOTE AMBAO HATUKUIONA, HUYU SI JUSTIN BIEBER NA SERENA GOMEZ?. INAMAANISHA WAMERUDIANA?
UKATILI : HAMMER Q, UNYAMA HUU ULIOUFANYA KWA MKEO, NI UJINGA NA UBWEGE ULIO NAO. NAHISI WEWE NI MTOTO NA UNA AKILI ZA KITOTO
Suruari ya Hammer Q ikiwa imetapakaa Damu
HAMMER Q.
Binafsi pia ni Mtanzania, na Ninaye mama Mzazi mwenye jinsia kama hiyo ya Mkeo Mpendwa Salha. Pengine hata Mama yako Mzazi ni Jinsia hiyo hiyo ya Salha. Au Unabisha?
Haki ya Mungu, amini usiamini, unabahati kubnwa sana, maana Tanzania hatujachukulia Kivile suala la "DOMESTIC VIOLENCE", lakini kama ingekuwa hivyo, binafsi ningemuona MPUMBAVU sana yule ambaye angekuja kukutolea dhamana kwa Ujinga na Unyama huu ulioufanya kwa Mkeo Salha.
Kama ulikuwa hauna akili juu ya hili,adhabu uliyoitoa kwa Mkeo ni zaidi ya Ukatili ambao hata mama yako angefanyiwa,ungemuona katili aliyemfanyia hivyo. Kama ni masualaya Makosa ndani ya Ndoa zenu au Mahusiano yenu, kuna njia mbadala za kuyatatua, l;akini sio Ufala huu ulioufanya.
wewe sio Muislam kabisaaaaa...ila inabidi ujione kama Kafir, hasa kwa Tukio hili uliolifanya.
Nakuona Bwege sana,na tena Mpumbavu usiye na Akili kufanya hivi. Kama utakuwa umechukia,Bora iwe hivyo ili ujue kuwa unaidajhririsha Jinsia ya Mama Zetu wazazi.
EXCLUSIVE: HATUTAKI ZAWADI ZA MTOTO
WAKATI KIBONGOBONGO tukililia zawadi pindi tunapopata watoto katika Famili zetu, Hahahaaa, Kim na Kanye wamesema "HAWATAKI ZAWADI ZA MTOTO " toka kwa Rafiki au Shabiki yeyote yule
Kwa Mujibu wa Mtandao wa Udaku wa TMZ, imekaririwa kwamba Mwanadada Kim Kardashian amesema kuwa, badala yake, zawadi ambazo walitakiwa kupewa toka kwa Mafanz wao, jamaa na hata Ndugu, basi zipelekwe katika hospitali ya LURIE CHILDREN'S HOSPITAL iliyoko ChicagoMrekani,ambako Mtu Mzima KANYE WEST alikulia
BREAKING NEWZ: MSIGWA ANAUWASHA MOTO SASA HIVI BUNGENI
Na Frank M.Joachim
MBUNGE wa Iringa Mjini kwa Ticketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa, hivi sasa yuko anauwasha moto akiwakilisha maoni ya Kambi ya Upinzani Bungeni katika Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii, kwa mwaka 2013/ 2014.
Katibu wa CCM, Abdallah Kinana na Mkewe wametajwa kuhusika na Udanganyifu katika Baadhi ya Hisa katika Idara ya Maliasili na Utalii, huku Makada Wengi wa CCM wakitajwa haswa katika ugawaji wa Vitalu kwa Kampuni mbali mbali.
BLACK TOUCHEZ ITAZIDI KUKUJUZA KWA KILA KITU
BIASHARA : SONGEA ITAKUMBWA NA HILI
Na Julius Konala
HALMASHAURI ya Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma ipo hatarini
kukumbwa na baa la njaa kutokana na baadhi ya wakulima kuanza kuvuna mahindi
mabichi yakiwa shambani na kuyauza.
Aidha tulipita maeneo mbalimbali ya masoko ya uuzaji wa
mazao ya mahindi likiwamo soko kubwa la Sodeco lililopo katika Halmashauri ya
Manispaa ya Songea mkoani humo na kushuhudia hali hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya
wafanyabiashara walisema hali hiyo inatokana na serikali ya mkoa kushindwa
kutoa vibali vya kununulia mahindi ya mwaka jana katika ghala la hifadhi ya
chakula la taifa.
Kwa upande wake mmoja wa wafanyabiashara ambaye pia ni
Mkurugenzi wa kampuni ya kukoboa na kusaga nafaka ya Mtanzamo, Julius Mlawa,
alisema lengo la serikali ya Mkoa wa Ruvuma kutaka kutoa vibali vya kununua
mahindi kwenye ghala la chakula la taifa kwa kipindi kile lilikuwa zuri, lakini
kwa sasa mpango huo hautafanikiwa kutokana na serikali kutaka bei ya sh 450 kwa
kilo moja wakati sasa wakulima wanauza sh 300 kwa kilo.
Alisema kwa ujumla wafanyabiashara mara zote wamekuwa
wakisukumwa na soko lililopo, kwani wakulima walishaanza kuuza mahindi mapya
tofauti na kipindi cha nyuma ambacho Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu,
alipoahidi kutoa vibali vya kununua mahindi kutoka hifadhi ya chakula ya taifa
ambapo mahindi mapya yalikuwa bado hayajaanza kuvunwa.
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Joseph Mkirikiti, amepiga marufuku
kwa wafanyabiashara wanaojihusisha na ununuzi wa mahindi mabichi kutoka kwa
wakulima na kusema kufanya hivyo ni kuwanyonya wakulima na kukaribisha janga la
njaa na kuongeza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mfanyabiashara
yeyote atakayebainika kufanya hivyo.
MAJANGA: MOROGORO MAFURIKO TENA
NAVicky Kombe, Morogoro
NYUMBA 25 na mashamba ya mazao ya chakula yanayokadiriwa
kufikia ekari 2908 katika kata ya Bwakira chini wilaya ya Morogoro, yamesombwa
na maji baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko.
Tukio hilo lililtokea Aprili 6 mwaka huo na kuvihusisha
vijiji vinne vya Bonye, Mbwade, Bwakira chini na Dakawa na hivyo kuwaacha
wakazi wake katika wakati mgumu.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Diwani wa
kata hiyo, Pessa Mohamed, alisema kuwa mafuriko hayo mbali ya kuharibu makazi
na mashamba ya mazao ya chakula, pia yameziacha familia 1598 zikiwa hazina
mahala pa kuishi.
Kwa mujibu wa diwani huyo, mazao yaliyoharibiwa na ekari
kwenye mabano kuwa ni mahindi (1158), mpunga (1143), ufuta (274), nyanya (3),
ufuta (27), alizeti (3) miwa (2) na nyanya (1).
Hata hivyo, alisema kuwa juhudi zinafanywa kuhakikisha
wakulima wanapata mbegu kwa kushirikiana na kitengo cha maafa katika wilaya
hiyo.
Alisema kutokana na mafuriko hayo, kata hiyo sasa inaweza
kukumbwa na njaa na hivyo ameiomba serikali na wadau mbalimbali kujitokeza
kusaidia mbegu za mahindi za muda mfupi kwa ajili ya kunusuru njaa katika kata
hiyo.
“Tunaomba wadau mbalimbali watusaidie mbegu za mahindi ya
muda mfupi kwanza kuliko kuleta chakula, hicho kitafuata baadaye,’’ alisema.
Subscribe to:
Posts (Atom)