Mustafa Abdel Akikabidhiwa Madaraka |
Na Frank M. Joachim & DW
Takribani mwaka mmoja tangu kuondolewa madarakani kwa
aliyekuwa Rais wa Libya Kanali Muammar Gaddafi, Baraza la Mpito nchini humo
limekabidhi madaraka kwa bunge jipya la nchi hiyo. Kwa heshima ya mwezi mtukufu
wa Ramadhani, sherehe za kukabidhi madaraka zilifanyika usiku wa jana. Muda
mfupi baada ya tukio hilo, nderemo na vifijo vilisikika kwenye mitaa ya mji
mkuu wa Tripoli huku fataki zikirushwa angani. Raia nchini humo wamesikika
wakisema kuwa "Libya itakuwa nchi huru na yenye demokrasia siku
zote". Bunge hilo lenye wabunge 200 litafanya kazi ya kumchagua Waziri Mkuu
ambaye ataunda serikali. Bunge hilo litatunga sheria ambazo zitaiweka Libya
kwenye uchaguzi kamili wa bunge baada ya kuandikwa kwa katiba mpya hapo
mwakani. Chombo hicho kilichaguliwa mwezi uliopita katika uchaguzi wa kwanza
huru na wa haki tangu kuondolewa kwa Gaddafi. Wabunge wanatoka kwenye vyama vya
siasa na wabunge wa kujitegemea.
EmoticonEmoticon