MKUU WA MKOA WA IRINGA, DR. CHRISTINE ISHENGOMA |
Iringa
Na Edwin Moshi
WAKATI maandalizi ya sensa ya
watu na makazi inayotarajiwa kufanyika usiku wa Agosti 25 kuamkia Agosti 26
mwaka huu yakiendelea kuchukua kasi hapa nchini , mkuu wa mkoa (RC) wa Iringa
Dkt Christine Ishengoma amepiga marufuku viongozi kuwa kuwasumbua wananchi kwa
michango kwa kipindi hiki cha kuelekea katika zoezi la Sensa ya watu na makazi.
Pia atangaza kumchukulia hatua
kali ya kisheria kiongozi yeyote ambaye atabainika kuomba fedha kutoka kwa wananchi
pindi anapokuwa katika majukumu yake ya kuhamasisha zoezi la sensa .
Dkt Ishengoma alitoa agizo hilo
leo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake na kudai kuwa ili
kufanikisha zoezi hilo la Sensa ya watu na makazi katika mkoa wa Iringa
amelazimika kusimamisha michango yote ya maendeleo kwa wananchi ili kuwaondoa
na hofu mbali mbali juu ya michango hiyo na badala yake kujiandaa kwa
kuhesabiwa pekee.
Hatua ya mkuu huyo wa mkoa wa
Iringa kupiga marufuku viongozi kuchangisha wananchi michango mbali mbali ya
kimaendeleo imekuja baada ya kuibuka kwa vitendo vya baadhi ya viongozi
kuidaiwa kupita kwa wananchi na kukusanya michango ya maendeleo huku baadhi ya
wananchi wakianza kuingiwa na hofu kuwa yawezekana viongozi hao wakatumia siku
hiyo ya sense kuwakamata kwa kushindwa kulipa michango.
Alisema kuwa ni vema kwa kipindi
hiki cha kuelekea katika zoezi hilo la sensa viongozi wa vijiji,mitaa kata na
wilaya kuachana na mpango wa kupita kwa wananchi kuchangisha michango hiyo ama
kuhamasisha juu ya wananchi kuchangia miradi ya maendeleo ili kuwafanya wananchi
hao kujiandaa kwa kuhesabiwa pekee.
EmoticonEmoticon