MOSHI |
MOSHI
Na Edwin Moshi
ZAIDI ya walemavu 200 wanatarajia
kunufaika na mafunzo juu ya namna ya kuwa wajasiriamali na namna ya kupambana
na virusi vya ukimwi.
Mafunzo hayo ambayo
yatawajumuisha walemavu wa viungo yanatarajia kuanza hivi karibuni kwa
kuzijumuisha wilaya tatu ikiwemo wilaya ya Rombo,Moshi vijijini na Manispaa ya
Moshi.
Akizungumza katika mahojiano maalumu
na kituo hiki ofisini kwake jana,Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la
Indigo Women Link lenye makao yake makuu jijini Dar es saalam dr.Rosemary
Daniel alisema lengo la kutoa mafunzo hayo kwa kundi hilo ni kutokana na kundi
la walemavu kusahaulika katika masuala mtambuka.
Dr.Rosemary amesema suala la
kumsaidia mlemavu kwa kumpatia mafunzo ya namna ya kujikwamua kiuchumi na kifikra
juu ya ugonjwa wa ukimwi na virusi vya ukimwi ambapo kutawawezesha kujikinga na
maambukizi mapya.
Ameongeza kuwa,kwa kuwapatia
mafunzo hayo,kutawawezesha kujiunga na kuanzisha vikundi vya biashara ndogondogo
kwa kuzingatia aina ya ulemavu walionao ili waweze kujipatia kipato.
Aidha amewataka viongozi wa kata na
vijiji kutoa ushirikiano kwa kuwapatia taarifa walengwa ili wote waweze
kushiriki mafunzo hayo na kuongeza kuwa matarajio yao ni kuwapatia elimu
walemavu zaidi ya 400 baada ya mafunzo ya awamu hiyo.
EmoticonEmoticon