Makete
Na Edwin Moshi.
Baadhi ya wakazi wa Makete mjini
wameipongeza serikali kwa kufanya ukarabati wa barabara za mitaa huku wengine
wakiukosoa uamuzi huo wa serikali
Wakizungumza na mwandishi wetu
wakazi hao wamesema zoezi hilo la ukarabati wa barabara hizo umekuja wakati
muafaka kani barabara hizo zimesahaulika kwa kutofanyiwa matengenezo kwa muda
mrefu hali iliyosababisha mitaro ya barabara hizo kuziba na maji kupita juu ya
barabara hizo wakati wa masika na kusababisha uharibifu mkubwa
Mmoja ya mkazi wa makete mjini
aliyejitambulisha kwa jina Obeth Sanga amesema kutokana na barabara hizo
kutofanyiwa matengenezo ya muda mrefu kumepelekea baadhi ya wakazi wa makete mjini
kumwaga vifaa vya ujenzi kwenye mitaro ya barabara hizo na kuviacha kwa muda
mrefu hali inayoharibu barabara hizo
“Hebu fikiria mtu unaleta mchanga
au mawe ya kujenga halafu unaviacha kweye mitaro kwa muda mrefu, mvua zikianza
maji yanakosa pa kwenda yanapita juu ya barabara na kuziharibu halafu wao wao
wanaanza lawama kwa serikali” amesema Sanga
Katika hatua nyingine wakazi hao
wameilaumu serikali kwa ukarabati huo na kusema umekuja wakati ambao kuna vumbi
hivyo zoezi hilo linazidi kuongeza vumbi
Monica Mahenge ambaye ni mkazi wa
Makete amesema ujenzi huo kwa hivi sasa hauna tatizo isipokuwa baada ya wiki
moja vumbi litazidi hivyo kuongeza adha kwa wananchi, hivyo ameshari ujenzi huo
ungesubiri angalau mwezi Novemba ambapo ni karibu na msimu wa mvua
“sawa wanamwaga maji kwenye hizi
barabara na vumbi linaondoka kabisa lakini baada ya wiki moja vumbi linajaa
kama mwanzoni, yaani ni bora wangesubiri karibu na masimu wa mvua ndio wajenge,
halafu kwa sasa magari mengi yanapita huku hayapiti kule kwenye barabara kuu
kwani wanakwepa matuta, yaani vumbi litatumaliza” alisema Bi. Monica
Halmashauri ya wilaya ya Makete
ipo kwenye utekelezaji wa kukarabati barabara za mitaa ambazo zimesahaulika kwa
mda mrefu, kama ilivyokuwa ikilalamikiwa na wananchi wengi kuwa barabara hizo
ni mbovu
EmoticonEmoticon