|
WANAJESHI WA NIGERIA |
|
RAIS WA NIGERIA, GOODLUCK JONATHAN |
Wanajeshi wawili wamepigwa risasi na kuuwawa na
washambuliaji walioufyetulia risasi msafara wao katika mji wa Okene katika
jimbo la Kogi nchini Nigeria. Msemaji wa polisi katika jimbo hilo ameliambisha
shirika la habari la AFP kuwa wanashuku mauaji hayo yamefanywa na wanaume
waliowaua waumini wasiopungua 19, katika kanisa moja la Kiinjili katikati mwa
Nigeria. Hapo jana maafisa walisema waumini hao waliuwawa wakati wanaume
waliokuwa wamejihami na bunduki walipolivamia kanisa hilo na kukata umeme kabla
kuanza kufyetua risasi wakati giza lilipotanda ndani ya kanisa hilo. Mashambulizi
ya jana ni mfululizo wa hivi karibuni wa mashambulizi ya risasi na mabomu dhidi
ya Wakristo nchini Nigeria.
Share this
EmoticonEmoticon