wananchi wakiwa katika ajali hiyo
gari la naibu waziri likiwa limepinduka
msamalia mwema kitoa msaada
mheshimiwa akiwa amejeruhiwa
Naibu waziri wa
Afrika Mashariki,Abdullah Juma Abdalla Saddallah na familia yake, wamekumbwa na
ajali mbaya eneo la Tumbi Kibaha wakati
akitoka Bungeni.
Ajali hiyo mbaya ilitokea majira ya jioni hii wakati naibu
waziri huyo akitokea Bungeni kuelekea jijini Dar es salaam akiwa na mkewe
pamoja na watoto wake wawili sanjari na dereva wake ambaye amejeruhiwa vibaya katika
ajali hiyo na kukimbizwa hospital yaTumbi-Kibaha.
Kwa Mujibu wa Mashuhuda wa ajali hiyo akiwemno imesemekana kuwa chanzo cha ajali hiyo Lori, ambapo dreva
wa Kiongozi huyo alikuwa akijitahidi kupishana nalo , hali iliyosababisha gari lake kuacha
barabara na kupinduka .
Shukrani za dhati ziwafikie wananchi ambao walikusanyika
katika eneo la tukio, katika jitihada za dhati za kuwazuia Vibaka kutokuiba
mali yoyote katika Gari hilo.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Nchini, Kamanda Mohamed
Mpinda, amethibitisha kutokea kwa ajali
hiyo
“Hali ya naibu waziri huyo si mbaya sana zaidi ya dereva
wake ambaye ameumia kichwani." Alisema Kamanda Mpinga
EmoticonEmoticon