Wakazi wa ufilipino wakiwa katika paa za nyumba zao, baada ya mafuriko. |
Timu ya waokoaji katika shughuli zao nchini ufilipino |
Na Frank M, Joachim
Mafuriko makubwa yamewaua watu wapatao 15 nchini Ufilipino.
Mafuriko hayo yanaelezwa kuwa mabaya kabisa kuwahi kuimbuka nchi hiyo tangu
mwaka 2009, huku maji yakifikia urefu wa mita moja unusu katika mji mkuu,
Manila. Makazi yalifunikwa na mafuriko hayo huku yakisababisha maporomoko ya
tope. Maelfu ya wakaazi wamelazika kuzikimbia nyumba zao, lakini wengi bado
wamekwama. Kampuni za umeme zimekata huduma za umeme baada ya maji kuingia
katika mitambo ya umeme, hivyo kuuacha mji wa Manila bila umeme. Kwa mujibu wa
idara ya utabiri wa hali ya hewa, mafuriko hayo yalisababishwa na upepo mkali
na mvua kubwa zilizonyesha nchini humo wiki iliyopita.
EmoticonEmoticon