viti vipya vya jengo jipya la bunge nchini kenya. viti hivi vimetengenezwa na kitengo cha magereza nchini humo |
Na Frank M. Joachim
Bunge la Kenya lililokarabatiwa na ambalo limekuwa gumzo
kubwa kwa sababu ya gharama ya viti vya bunge hilo, hatimaye limefunguliwa
rasmi na rais wa nchi hiyo Mwai Kibaki.
Viti hivyo vimegharimu dola 3,000 za kimarekani kwa kila
kiti kimoja vikiwa jumla ya 350 vimetengenezwa na kitengo cha magereza nchini
humo.
Zabuni ya kwanza ya kutengeneza viti hivyo ilitolewa kwa
kampuni moja ya nje lakini ilifutwa baada ya baadhi ya wabunge kugundua kila
kiti kingegharimu dola 5000 za kimarekani.
Maafisa wanasema ukarabati huo uliogharimu dola milioni 12
utaliweka bunge katika mfumo mpya wa kisasa wa komputa.
Je, sisi viti vyetu vilitengenezwa na kitengo kipi....hapa nchini
EmoticonEmoticon