Mji Mkuu Wa India, New delhi.
Moja kati ya Mitaa ya India.
Na Frank Joachim & DW
NEW DELHI, India.
Umeme umeanza kurejea
asubuhi ya leo , jumatano, baada ya majimbo
20 kati ya
28 nchini India , pamoja na
mji mkuu wa New Delhi, kukumbwa
na kukatika kwa
umeme.
Magridi matatu makuu
kati ya
matano ya kusafirishia
nishati hiyo yalishindwa kufanya kazi. Hali hiyo ni ya pili
kutokea katika muda wa
siku mbili, na imesababisha
zaidi ya watu
milioni 600 kubaki bila umeme. Mfumo wa
usafiri ulishindwa kufanyakazi, hospitali zililazimika kutumia
umeme mbadala wa genereta na
mamia ya wachimba migodi
walikwama chini ya
ardhi kwa kuwa
lifti hazikufanyakazi.
Matukio
hayo mawili yaliyofuatana
ya kukatika umeme
siku ya jumatatu na
jumanne yamezua wasiwasi
mkubwa juu ya
miundo mbinu nchini India
na uwezo wa
serikali wa kukabiliana
na mahitaji ya nishati
wakati India inajaribu
kuwa dola kuu ya kiuchumi
duniani.
EmoticonEmoticon