Na Frank Joachim
Kampala, Uganda
Nchini Uganda ,
shirika la afya
ulimwenguni limeripoti kuwa
watu 36 upande wa
magharibi ya nchi
hiyo wanashukiwa kuwa wanaugua
ugonjwa wa Ebola, ugonjwa ambao
huambukiza na ambao umesababisha
vifo vya watu
14.
Wizara ya afya
nchini Uganda imetangaza rasmi
kuzuzka kwa ugonjwa
huo katika wilaya ya Kibaale
siku ya
jumamosi na kusema
kuwa watu 20 wameambukizwa. Shirika hilo
la afya ulimwenguni , WHO, limethibitisha kuwa
hakuna mtu aliyeambukizwa nje
ya wilaya hiyo ya
Kibaale, na kwamba
haihitajiki kwa sasa
kuchukuliwa hatua za kudhibiti
biashara na usafiri kwendea
Uganda.
Hakuna matibabu
ama chanjo kuutibu ugonjwa huo,
na ni
mara ya nne ugonjwa
huo wa Ebola
kuzuka Uganda tangu
mwaka 2000, ambapo watu
224 walifariki.
EmoticonEmoticon