Na Frank M. Joachim
Habari kutoka Madagascar zinaarifu kuwa, watu 9 wameuawa
katika mapigano yaliyozuka kati ya polisi na watu wenye silaha kusini mwa nchi
hiyo.
Duru za habari zinaaru kuwa, 6 kati ya watu hao waliouawa walikuwa
miongoni mwa wanachama wa kundi hilo lililokuwa na silaha, huku wengine 3
wakiwa wakiwa wanajeshi. Hadi sasa makumi ya watu wamekwishauawa katika
ufyatulianaji risasi kati ya wanajeshi na watu wenye silaha ambao wanajihusisha
na wizi nchini Madagascar.
Ni vyema kuashiria hapa kwamba, Madagascar imekuwa
ikikabiliwa na hali ya mchafukoge tangu kulipotokea mapinduzi ya kijeshi
yaliyomng'oa madarakani rais wa nchi hiyo miaka minne iliyopita.
EmoticonEmoticon