Na Frank M. Joachim
Ndege za kijeshi zisizo na rubani za Marekani zimetekeleza
shambulio nchini Yemen na kuua watu wasiopungua 13.
Hayo yamethibitishwa na
kingozi mmoja wa ngazi za juu wa Yemen ambaye hakutaka jina lake litajwe
na kuongeza kuwa, shambulio hilo lililofanywa na ndege za Marekani zisizo na
rubani, lilifanyika hapo jana dhidi ya watu wanaodhaniwa kuwa na mahusiano na
mtandao wa kigaidi wa Al-Qaida.
Amesema kuwa, shambulio hilo halikuweza kupiga
eneo husika na badala yake lililenga magari mawili ya raia katika mji wa Radda
unaopatikana katika mkoa wa Al Bayda ambapo watu 13 waliuawa papo hapo wakiwemo
wanawake wawili na wengine wakijeruhiwa vibaya.
Wananchi wa Yemen wamekuwa
wakipinga vikali uingiliaji wa Marekani nchi mwao sambamba na kufanya
maandamano makubwa huku wakitoa nara za "Mauti kwa Marekani, Mauti kwa
Israel." Mbali na Wayemeni hao kupinga uingiliaji wa Marekani nchini kwao,
wanapinga na kulaani mashambulizi ya ndege hizo zisizo na Rubani nchini humo
ambayo mwezi uliopita yaliua idadi kubwa ya raia wasio na hatia.
Hivi karibuni
Rais Barack Obama wa Marekani alijigamba akidai kuwa, kila Mmarekani anaona
fakhari kwamba nchini yake ina nguvu na inaheshimiwa kwa kuendesha vitani zaidi
duniani.
EmoticonEmoticon