Na Frank M. Joachim
Duru za usalama nchini Libya
zimetangaza habari ya kutiwa mbaroni wanamgambo wenye silaha wanaoaminiwa kuwa
ni mabaki ya utawala wa Kanali Muammar Gaddafi uliopinduliwa nchini humo.
Watu
hao wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kushambulia maeneo nyeti na muhimu ya mji wa
bandari wa Sirte wa kaskazini mwa Libya pamoja na kupanga kufanya mashambulizi
katika maeneo mengine ya nchi hiyo.
Shirika
rasmi la habari la Libya (WAL) limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, maafisa
usalama wa nchi hiyo wamewatia mbaroni watu kadhaa ambao inaaminiwa ni wafuasi
wa utawala uliopinduliwa wa nchi hiyo na ambao walifanya mashambulizi katika
maeneo muhimu ya mji huo.
Kwa
mujibu wa ripoti hiyo, miongoni mwa maeneo muhimu yaliyoshambuliwa na
wanamgambo hao ni kituo cha kuzalisha umeme cha az Zaafaran ambacho kinazalisha
umeme wa mji wa Sirte. Maafisa usalama wa Libaya wamesema kuwa, watu hao walikishambulia
kwa roketi kituo hicho.
EmoticonEmoticon