Na Baba Juti
MTANDAO wa Facebook umekutana na tuhuma nyingine za kutoa matangazo ya ajira ambayo kwa asilimia kubwa yamekuwa yakionekana kuwa na ubaguzi wa “kijinsia”
Kwa mujibu wa mashtaka hayo mapya yaliyofunguliwa na Taasisis mbili ambazo ni ACLU na Equal Employment Opportunity Commission, inasemekana kuwa Matangazo mengi ya ajira ambayo huwa yanapostiwa Facebook, yamekuwa yakikiuka Haki za Ajira kwa sababu Waajiri wengi huonekana kupendekeza na kutangaza nafasi za kazi kwa jinsia ya kiume tu na sio ya kike kwa wingi
Aidha, Pia Taasisis hizo zimeweka wazi orodha ya Waajiri/Makampuni 10 ambayo yamekuwa yakitoa nafasi za kazi kibaguzi hasa wanawake wakiwa ndio waathirika wakubwa.
Makampuni ama waajiri 10 ambao wametajwa kutangaza nafasi za kazi zenye ubaguzi wa kijinsia katika Mtandao wa Facebook ni pamoja na Abas USA, Defenders, Nebraska Furniture Mart, City of Greensboro North Carolina, Need Work Today, Renewal by Andersen LLC, Rice Tire, JK Moving Services, Enhanced Roofing & Modeling and Xenith.
Uongozi wa Mtandao wa Facebook umeweka wazi kuwa, wao kama njia ya kuunganisha watu wote ulimwenguni katika suala la mawasiliano, hajaruhusu na wala hawakubaliani na “Ubaguzi” wa aina yoyote katika mtandao huo, na wako tayari kufuatilia kile kinachodaiwa ili wachukue hatua haraka iwezekanavyo