Na Baba Juti
#WatuWaMungu naamini kabisa kuwa mnakumbuka ule muunganiko wa T-Pain na Lil Wayne uliofahamika kwa jina la T-WAYNE
Wawili hawa walipata kuchukua akili za wengi kupitia Mkwaju Korofi mpaka leo, unaofahamika kwa jina la GOT MONEY, na kila mtu kuvutiwa zaidi na Video hasa namna ambavyo ilisukwa
Sasa Basi, T-Pain ama Nappy Boy, amedai kuwa anahitaji kulipwa mkwanja ambao ni USD 500,000 sawa na Tsh 1,083,500,000 ambazo anadai hakulipwa baada ya kufanya naye kazi katika album yake ya THE CARTER III
Kazi hiyo ambayo ilifanyika kwa Takriban miaka 10 iliyokata, inadaiwa kufanyika katika Recording Label ya T Pain ambayo inafahamika kwa jina la NAPY BOY RECORDS na T Pain mwenyewe ndiye alikuwa Producer wa Kazi hiyo.
Ukiachilia mbali suala hilo, T Pain anadai kuwa, baada ya Mkwaju huo kufanikiwa na kushika akili za walimwengu wengi, hakuvuna mkwanja wowote na badala yake amekuwa akipigwa Chenga kwa asilimia kubwa
Mbali na hilo, madai mengine yanaongeza kuwa, Msanii kutoka Nappy Boy Records, anayeitwa YOUNG FYRE, alihusika kuazima baadhi ya mawazo katika Production ya mkwaju mwingine unaoitwa HOW TO HATE akiwa pia amemshirikisha T Pain, hivyo inahitaji kulipwa kiasi hicho cha fedha
Mpaka hivi sasa, Lil Wayne ama uongozi wa Young Money haujaweka bayana kama Deni hilo wanalitambua ama Lah
EmoticonEmoticon