REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

UTAFITI: MTUMIAJI WA POMBE ANAWEZA KUJIFUNZA KUTUMIA LUGHA NYINGINE (YA KIGENI) KWA UFASAHA ZAIDI

2:47:00 AM

Na baba Juti
UCHUNGUZI umefanyika na kubainika Kuwa Unywaji wa Pombe unaweza kumfanya Mtu akazungumza Lugha za mataifa Mengine

Uchunguzi huo umebaini kuwa, unywaji wa Pombe kiasi fulani (hasa Kidogo) kinaweza kumfanya Mtumiaji akawa na ujuzi wa Lugha Nyingine hasa kutoka mataifa Mengine

Team ya Utafiti Kutoka Liverpool Uingereza, Vyuo Vikuu vinavyofahamika kwa Majina ya MAASTRICHT UNIVERSITIES,  Na KING'S COLLEGE zilitoa taarifa kuwa, unywaji wa Pombe husababisha athari ama hudhuru sehemu kadhaa za binadamu ikiwemo Nguvu ya Kufanya kazi kwa Ubongo, na Nguvu ya Mwili.

Tofauti na hayo, Ilidaiwa kuwa kupoteza kumbu kumbu, kukosa nguvu na uwezo wa Kufikiria, lakini pia uvivu wa kimwili, husababishwa na Unywaji wa Pombe

Ila sasa, kuna faida mpya ambayo imebainika safari hii, kuwa kunywa Pombe kunaweza kumfanya Binadamu akatumia Lugha zaidi ya Moja hasa zile kutoka Nje ya Nchi ambayo binadamu husika anatumia Lugha yake Mama au ya kitaifa.

Pia watafiti hawa Wapya wameongeza kuwa, Pombe hujenga Ujasiri Binafsi kwa Mtumiaji na hata kutumia Fursa hiyo kuzungumza na mwenzake ama wenzake ama Wenyewe Lugha Nyingine za Kigeni zaidi kuliko hata Lugha yake Mama

Hivyo, kwa utafiti wa Awali, imegundulika kuwa, Mtumiaji wa Pombe kwa kiasi fulani, hata kama hajui, huweza kukusanya hata maneno mawili matatu licha ya kuchapia katika lugha ya kigeni, lakini atazungumza na kueleweka kwa kiasi Fulani


Pia Mtumiaji wa Pombe, hupendelea mara kwa mara kutumia Lugha Nyingine tofauti na ile ambayo huizungumza siku zote katika Majukumu yake ya kila siku

Mmoja kati ya Watafiti, Dr. Inge Kersbergen kutoka Chuo Kikuu cha Liverpool, taasisi ya Saikolojia, Afya na Jamii alisema Hivi, tunamnukuu
" Utafiti wetu unaonesha kuwa unywaji wa Pombe, unaweza kuwa na manufaa katika kutamka maneno ya Kigeni hasa kwa wale ambao anagalau wameshajifunza Lugha hiyo. Hii pia husaidia ama huleta faida ya kujifunza zaidi hasa ukiizungumza ukiwa na wale ambao wanaifahamu lugha husika kwa ufasaha zaidi"

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER