Na Rich Sam WAUNGWANA wameamua kumfanya Nicki Minaj apate Hasira za kutosha mpaka kutangaza Dau la USD 100,000 kwa yeyote atakayempatia Ushahidi ambao mpaka hivi sasa umemuweka katika wakati mgumu hapa Duniani aisee
Hitmaker Huyu wa "ANACONDA" alijikuta akimiminiwa "Ndimu" za Kutosha ikiwa ni baada ya kudaiwa kuwa aliropoka kwamba yeye ndiye kawafanya Wasanii Wote wa Rap kwa Jinsia ya Kike wawe katika Ramani ya Muziki, kitu ambacho kwa upande wake amekikanusha na kuamua kuandika walaka Mrefu sana kupitia Instagram account Yake.
Katika Post alioipost bibie huyu baada ya kukutana na janaga hilo, aliandika kuwa, anahitaji kuweka sawa kuhusu kauli hiyo ambayo imenukuliwa Tofauti na Mitandao ya Kijamii na Tv Station mbali mbali, huku akimtaka yeyote yule atakayeona "nukuu" hiyo, basi amcheki na kumpatia USD 100,000.
Tunamnukuu tafadhari NICKI MINAJ
"Ninanona Watu wana-remix maneno yangu, hivyo ngoja nipost kile nilichokisema haswa kwa wale ambao wana uelewa. Sasa, kama utapata Sehemu ambayo nilisema "Nimewafanya Rappers wa Kike kuwa katika Main Stream", nitakupatia USD 100,000. Blogs na Tv shows mbali mbali huwa hawajalishi utafiti, huwa wanajali kuchukua hisia zako. Hebu fikiria mie kusema nimewaweka katika Ramani ya Muziki rappers wa Kike wakati kuna wengi ambao tayari walishaingiza albums zao Platnum kupitia Nguvu zao. Lauryn mpaka nakala Milion 10 ya moja kati ya Albam zake. Eve alikuwa na Nyimbo zilizogusa Pltnum akiwa na Alicia Keys, Gwen Stefani, Tv Show yake na Mavazi yake, Missy Eliot Pia Nyimbo zake. Foxy Brown na Lil Kim walikuwa Album ambazo ziliingia Pltnum na walitengeneza vizuri Sound ya Wasanii wa Kike wanao Rap kutoka New York. Akina Queen Latifah, Trina naye alikuwa na Album ambayo ilifika mpaka Billboard. Ninapenda sana upendo wa watu lakini sijawahi kusema hivyo.........."
EmoticonEmoticon