Na Baba Juti
#WatuWaMungu kwa kumbu kumbu zetu,. Tumewahi kuwaambia kuwa
mamito BEYONCE aliwafikisha Mahakamani wamiliki wa Mtandao mmoja ambao umekuwa
ukitumia Sehemu ya Jina lake na Kazi zake kuzalisha Bidhaa kinyume cha
Utaratibu.
ILIKUWAJE?
BEYONCE alifungua Mashtaka Dhidi ya Wafanya biashara Wawili
ANDRE MAURICE na LEANA LOPEZ ambao walikuwa wanamiliki wa kampuni ya MERCH
ambao walikuwa wanatengeneza bidhaa mbali mbali zenye jina la FEYONCE ambalo
linatokana na kila kitu cha Jina lake la BEYONCE hasa lilivyotumika katika
album yake aliyoipa jina la BEYONCE
Kampuni hiyo ilikuwa inazalisha vitu kama Vile TISHRT za
Kike na Vitu vinginevyo, lakini wakitumia Logo Hiyo. Tofauti na hilo, walianza
kuzalisha Tshirt na Bidhaa nyingine zenye maneno ya PUT A RING ON IT, maneno
ambayo yalitumika katika wimbo wa Beyonce unaoitwa SINGLE LADIES
WANACHODAI WATUHUMIWA
Kwa Mujibu wa Malalamiko yao Mapya, Wawili hao kutpoka
kunako Kampuni hiyo, wanadai kuwa BEYONCE amekuwa akiwakandamiza sana katika
Kesi hiyo kitu ambacho kinawanyima Uhuru wa kufanya Vitu vyao vingine
Mnamo May 11, wawili hao walidai kwamba wamefanya kila
liwezekanalo kufuta matangazo ya Bidhaa hizokwenye website ambayo inatangaza bidhaa hizo ingawa bado
inakuwa Ngumu
Ukiachilia hilo, Wawili hao wanazidi kudai kuwa Beyonce
amekuwa akitumia Jina lao kuzuia Riziki ambazo zinakuja kwao, kitu ambacho
kimewakosesha Fedha Nyingi sana mpaka Hivi Sasa
Hivyo, wanaomba Mahakama Kupiga Chini Kesi hiyo ili wafanye
Shughuli zao Nyingine
EmoticonEmoticon