Na Baba Juti
#WatuWaMungu kama kuna wale Watoto wa Kike hapa Nchini
Tanzania huwa wanajichubua na Kujiongezea Mvuto hasa kimaumbile kwa sababu ya
kuvutia wanaume ama kufuata Mkumbo, basi tumieni akili sana, Kenya wanawafunika
kupita Maelezo
Wanawake Wengi Nchini Kenya, hutumia Gharama Nyingi sana
kuboresha Muonekano Wao, kitu ambacho wao kama wao wanadai kuwa kinarudisha
Gharama hizo walizotumia pamoja na kupata Faida Juu.
VERA SIDIKA, binti ambaye mara Nyingi hutolewa Mfano katika
Kujichubua na Kuongeza Maumbile ya Mwili wake hapa Afrika Mashariki, yeye ni
mmoja kati ya Wale ambao hawajutii kufanya hivyo sababu kuna Vitu vingi sana
ambavyo anafaidika Navyo kutokana na hatua yake
Akifafanua kuhusu Kile ambacho kinaendelea Juu yake, Vera
anadai kuwa, yeye kama yeye, alijichubua na hata kuongeza Ukubwa wa Matiti na
makalio, ila ni kwa sababu ya faida ambayo ameipata Mpaka Hivi sasa
Vera amedai kuwa, Tangu amejichubua, basi ameng’arisha Brand
yake na alifanya hivyo kwa sababu
alitaka aishi maisha ya Furaha ambayo anayataka
Katika faida aliyopata, Vera anadai kuwa ameweza kuhost
Events Nyingi ambazo zimepatikana kutokana na Muonekano wake, Amepata Watu
Wengi ambao wanamfuatilia, Bookings Nyingi za Events, Dili Nyingi sana za
Kibiashara ambazo zinamjia mpaka hivi sasa, Kufanya Kazi na makapuni makubwa ya
Kibiashara, na bado anashughulikia Kipindi chake Cha TV , pamoja na mambo Mengi
ambayo yako Njiani
Lakini katika Suala Zima la Kuboresha Muonekano wake, VERA
anadai kuwa Ilimgharimu almost Shilingi za Kenya Milioni 15, nab ado watu
walikuwa wanahisi kuwa hatofika Mbali na atakuwa ameshaharibika, ila mambo
yamekuwa Tofauti
EmoticonEmoticon