Na Baba Juti
#WatuWaMungu RAPPER Drake yuko
katika hati hati za kupandishwa Mahakamani endapo hatokubali kuwa Yeye ni baba
Halali wa Mtoto wa Mwanamke Mcheza Ngono maarufu aliyestaafu, SOPHIE BRUSSAUX.
Taarifa Mpya ambazo Team Hit Zone tumezinyaka Mpaka Hivi
sasa, Drake amepewa Muda Mchache sana ili kukubali na kukiri kuwa yeye ni baba
halali wa Mtoto na atatoa Mahitaji Maalum ya Mtoto kitu ambacho ni muhimu
kuliko yote sababu yeye ni moja kati ya wahusika wakubwa katika Ujauzito
alioupata Bibie huyo
Mpaka Hivi sasa, Sophie ameshatangaza Rasmi mwanasheria
ambaye atasimama naye katika kuhakikisha kuwa Drake anafikishwa Mahakamani kama
atakana kitu amcho kinaonekana Dhahiri kabisa kuwa motto huyo ni mali halali ya
Drake
Mwanasheria huyo anatambulika kwa jina la RAOUL FELDER.
Ukiachilia mbali taarifa mpya hizi ambazo tunazimimina
kwako, Drake aliwahi kuzungumziwa sana hasa kwa Kuwa Karibu na Sophie kipindi
ambacho amepigana Chini na Mwanamama J-Lo, hali ambayo inathibitisha kuwa
inawezekana kabisa Drake akawa alikunjuka na Mwanamama Huyu
Tofauti na Hilo, Sophie alianika wazi Mesej ambazo zilikuwa
zikimuonesha Drake akimlazimisha Bibie huyo kutoa Mimba Yake, kitu ambacho
Sophie hakukifanya hata Kidogo
EmoticonEmoticon