Na Baba Juti
KAMPUNI inayojishughulisha na Biashara ya Vito vya Thamani
a.k.a “Bling Bling”, imeamua kumburuza Mahakamani Rapper T.I ili awalipe
mkwanja wao wa Takriban USD Million 1 sawa na Tshs 2,285,000,000.
Kwa Mujibu wa Mashtaka hayo, Kampuni hiyo inadai kuwa T.I
mnamo Mwaka 2015, alikiuka Masharti ya Mkataba wao ambao walikuwa wamekubaliana
kibiashara, huku mara ya Mwisho akichukua Bling Bling zenye thamani ya USD
75,000 sawa na Tsh 171,375,000
Ingawa T.I alionekana kukana Mashtaka na Madai hayo kutoka
kwa Kampuni hiyo, wao wanadai kuwa walikuwa wakimuuzia T.I Vito vya thamani
vingi sana na vilivyowagharimu kwa asilimia kubwa. Biashara hiyo ilianza Mwaka
2004 mpaka 2012 ikiwemo Chain, Saa,Dog Tags za Diamonds.
Tofauti na hivyo, T.I anatuhumiwa pia kuchukua Vito vya
thamani vya Diamonds kwa ajili ya Mwanamke, ingawa hatujui kama ilikuwa ni kwa
ajili ya mkewe ama Lah
Kampuni hiyo ya Madini inaongeza kuwa, Awali T.I alikuwa
akiwalipa Vizuri tu kupitia Open Account ambayo walikuwa nayo, lakini ghafla
alistop kufanya malipo Mwaka 2013
Na Mmiliki wa Kampuni hiyo, FEYZ AYDIN anadai kuwa,
alijitahidi kwa kila mali kumkumbusha T.I kulipa Mkwanja wao, lakini hakukuwa
na Mafanikio, na Ndipo walipoamua kufungua Mashtaka Dhidi yake
EmoticonEmoticon