REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

AKAUNTI FEKI ZINAZIDI KUWATAFUNA WASANII WA BONGO INSTAGRAM

2:46:00 AM





INSTACOP, @instacoptz
MNAMO mwezi uliopita TTM tulikupa Mtonyo kuwa, Kuna Mtu kunako Mtandao wa INSTAGRAM anatumia Jina la WEMA SEPETU kuweza kufanya Utapeli wa hali ya Juu…

Sasa This Time Yule Presdaa wa wa Masharobaro, BOB JUNIOR, amekutana na Noma Hilo hilo, ambapo kuna Tapeli anatumia Jina lake katika Mtandao huo wa Instagram , kufanya Utapeli wa Nje Nje.

Rafiki wa Karibu wa Bob Junior, KITALE, ndiye ambaye amebombulua noma hilo, baada ya kutoa Info kuwa, tapeli huyo anajiita SHAROBARO BOB JUNIOR (@sharobarobojunior) akitumia uhalisia wa BOB JUNIOR TZ (@bobjuniortz).


Kitale ameongeza Kuwa, mtu huyo hivi sasa anafollowers wengi sana, na mara Nyingi amekuwa akitumia Picha na kila kitu anachokifanya Bob Junior, ili kuwafanya Bandugu waamini kuwa Ni Yeye.

Aidha jambo ambalo limemshtua sana KITALE, ni baada ya Bob Junior Feki kumtumia Meseji katika INSTAMESSAGE, na kumwambia amtumie 70,000 sababu amekwama, na yuko Kahama katika Show.

Tofauti na hilo, Bob Junior Feki amekuwa akiwatukana Mashabiki wa Bob junior hasa pale wanapocomment jambo fulani

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER